Halmashauri zilizofanya vibaya kwa kuandikisha chini ya Asilimia 50 hadi kufikia Tar 14/10/2019 ni
Moshi Manispaa - 31%,
Jiji la Arusha - 32%,
Nsimbo Dc - 41%,
Kigoma Manispaa - 43%,
Korogwe Mji - 45%,
Jiji la Mbeya - 46%,
Babati Mji - 46% na
Manispaa ya Musoma - 49%.
Selemani Jafo
Waziri wa Nchi, OR- TAMISEMI
15/10/2019
Tuesday, October 15, 2019
Sunday, March 10, 2019
Waziri Jafo: ‘Hatutaki ziro shule za vipaji maalum’
Waziri Jafo: ‘Hatutaki ziro shule za vipaji maalum’

Tabora Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo alisema hakuna sababu kwa wanafunzi wanaosoma shule za vipaji maalum kupata alama ya ziro au daraja la nne kwenye mitihani yao ya mwisho badala yake wanafunzi hao wanapaswa kusoma kwa bidii ili waendane na sifa halisi ya shule hizo. Akizungumza jana mara baada ya kuzitembelea shule za wanafunzi wenye vipaji maalum za wavulana na wasichana za Tabora zilijukanazo kama ‘Tabora Boys’ na ‘Tabora Girls’ Waziri Jafo alisema kutokana na wanafunzi hao kuchaguliwa kwenye shule za vipaji maalum wanapaswa kusoma kwa bidii ili wafaulu kwa alama za daraja la kwanza na la pili na siyo vinginevyo.
Alisema kuwa hakuna sababu kwa wanafunzi wanaosoma shule za vipaji maalum nchini kuendelea kubaki kwenye shule hizo endapo viwango vya wanafunzi hao kwenye matokeo yao ya mitihani ya majaribio yataonyesha kuwa na ufaulu wa kawaida. “Kuanzia sasa nawaagiza wakuu wa shule za vipaji maalum kuwapeleka katika shule za kawaida wanafunzi wote walio katika shule za vipaji maalum ambao matokeo ya mitihani yao ya majaribio itaonyesha kuwa na ufaulu wa chini,” alifafanua Waziri Jafo na kuongeza: “Hatuhitaji mwanafunzi wa shule ya vipaji maalum apate division (daraja) III na kuendelea, endapo kwenye mtihani wake wa majaribio wa kidato cha pili atapata ufaulu hafifu, ina maana mwanafunzi huyo hastahili kuendelea kukaa kwenye shule hiyo.” Kwa mantiki hiyo Waziri Jafo alieleza kuwa kuanzia sasa kwenye shule zote za vipaji maalum watabakizwa wanafunzi waliofaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza na la pili kwenye mitihani yao ya kidato cha pili na wanafunzi watakaofaulu kuanzia daraja la tatu na kuendelea watapelekwa kwenye shule za sekondari za kawaida.
Kadhalika kwa wanafunzi wa kidato cha tano wanaochaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalum wanapaswa kudhihirisha vipaji vyao kwa kuonyesha ufaulu wa daraja la kwanza kwenye mitihani yao ya kidato cha sita kama ilivyokuwa katika miaka ya 90 kurudi nyuma. Akiwa katika shule ya wavulana Tabora, Mhe.Jafo alionyesha masikitiko yake kutokana na kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa shule hiyo kuwa chini kiasi cha kuzidiwa na shule ya wasichana Tabora. Aliwataka walimu na wanafunzi wa shule hiyo kuongeza bidii ili shule hiyo iipite shule ya wasichana Tabora na endapo shule hiyo itafanya vizuri kwenye mitihani ijayo ya kidato cha sita, Mhe Jafo ameahidi kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali yajayo ya wanafunzi wa kidato cha nne yatakayofanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
Kwa upande wa shule ya wasichana Tabora nayo amewataka kuongeza bidii kwenye ufaulu wa mitihani ya kidato cha sita na kuwaahidi kugharamia chakula na pia kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne na pia kuwaalika wanafunzi wote wa kidato cha sita na wazazi wao endapo matokeo yajayo ya kidato cha sita, shule hiyo itafanikiwa kuwemo katika sita bora kitaifa. Mbali na kuzungumza na walimu na wanafunzi, Mhe.Jafo alipata fursa ya kujionea miundombinu iliyoboreshwa katika shule hizo ambapo kwa upande wa shule ya wavulana Tabora zaidi ya shilingi milioni 900 zilitumika kwenye ukarabati wa majengo ya shule hiyo ikiwemo ujenzi wa jengo la kisasa la maktaba ya shule hiyo.
Hata hivyo Mhe.Jafo alieleza kutoridhishwa kwake na kiasi kikubwa cha fedha kilichotumika kwenye ujenzi wa maktaba hiyo ambapo alisema kutokana na kiasi kilichotengwa kuwa kikubwa kilipaswa kutumika kwenye maktaba na miundombinu mingine Aidha Mhe.Jafo baada ya kutembelea miundombinu ya shule hiyo na kujionea ukarabati mkubwa uliofanyika alimwagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha kuwa kuanzia sasa fedha zote zitakazopelekwa kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe 25 zilizochaguliwa ahakikishe kuwa shule hizo zinatumia mfumo wa 'force account' ili thamani ya fedha iendane na ukarabati wa majengo.
Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Bwana Tixon Nzunda aliwataka walimu na wanafunzi wa shule hizo kusoma kwa bidii kwani serikali ya awamu ya tano imetoa kipaumbele kwenye sekta ya elimu. Aliongeza kuanzia sasa anatarajia maafisa elimu wa wilaya na mikoa watazingatia kuwapendekeza walimu walioonyesha bidii kufaulisha kwa kiwango cha juu ili waweze kupandishwa vyeo. Wakati huo huo Bwana Nzunda alisema kuwa zaidi ya wanafunzi 100 waliokuwa wakisoma katika shule za vipaji maalum wakiwemo wanafunzi 11 kutoka shule ya wasichana Tabora wamepelekwa kwenye shule za kawaida baada ya kutofanya vizuri kwenye mitihani yao ya kidato cha pili. Shule za wavulana na wasichana za Tabora ni miongoni mwa shule zinazochukua wanafunzi wenye vipaji maalum kama zilivyo shule nyingine za aina hiyo za Mzumbe, Kibaha, Ilboru, Kilakala, na Msalato ya Dodoma

WATU 159 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINES
BREAKING: Ndege ya Ethiopian Airlines yaanguka ikitokea Addis Ababa kwenda Nairobi, watu 15 waripotiwa kufariki Dunia.
Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, aina ya Boeing 737 MAX imeanguka leo asubuhi Marchi 10, 2019 ikitokea Addis Ababa, Ethiopia kwenda Nairobi Kenya.
Tayari Ofisi ya waziri Mkuu wa Ethiopia, imetuma salamu za rambi rambi kwa familia zilizopoteza ndugu zao kwenye ajali hiyo
Friday, March 1, 2019
EDWARD LOWASA ARUDI CCM
Waziri mstaafu na aliyekuwa mgombea wa Uraisi kwa tiketi ya CHADEMA Edward Lowasa ametangaza rasmi leo tarehe 01.03.2019 kuamua kurudi rasmi CHAMA CHA MAPINDUZI.
Uamuzi huo ameotoa mbele ya Raisi John Pombe Joseph Magufuli makao makuu ya chama mkoani Dar es salaam,``Nimerudi Nyumbani``ni maneno aliyosema Edward Lowasa leo hii.
Kwa maelezo na taarifa kamili usiache kutembelea ukurasa wetu.

Thursday, February 28, 2019
HISTORIA FUFI KUHUSU MAISHA NA UBABE WA ADOLF HITLER
ADOLF HITLER
Alikuwa dikteta wa Ujerumani kuanzia mwaka 1933 hadi kifo chake.
ADOLF HITLER AKIWA MTOTO
Alizaliwa nchini Austria katika mji wa Braunau am Inn karibu kabisa na mpaka kati ya
Ujerumani na Australia 20,april 1889 katika familia ya Alois Hitler na Clara Hitler,Alois
Hitler ambaye ni baba yake Hitler [1837-1903] alikuwa ni mtoto haramu wa Maria
Anna schicklgruber. mnamo mwaka 1842 Maria Anna aliolewa na Johann George Hiedler,
baada ya kifo cha mama yake[1847]na baba yake wa kufikia ambaye ni Johann Hieldler [1856]
Alois Hitler aliendelea kukua katika familia ya ndugu wa Johann aliyeitwa [Johann Nepomuk Hiedler.
mwaka 1876 alihalalishwa na viongozi wa dini kuwa ni mtoto halali wa Johann Nepomuk Hiedler na
akapewa jina jipya la George Hitler ambapo maana ya HITLER ni mtu aliyeishi ndani ya nyumba. Kuhusu
baba yake halisi wa George Hitler bado ni kitendawili kwa kuwa inasemekana kuwa mama yake Maria Anna
alikuwa ni mtumishi wa ndani katika familia ya KIJEWISHI, na kijana wa miaka 19 aliyeitwa Leopold Franknberger
katika familia hiyo alimbaka Maria na kuzaliwa Alois Hitler na ndio sababu akaitwa mtoto haramu,
hata hivyo taarifa za kuaminika juu ya Leopold bado hazijapatikana
HISTORIA ADOLF HITLER
Adolf Hitler alikuwa mtoto wa sita katika familia ya Alois Hitler na Clara Polz japo
MAMA YAKE HITLER CLARA HITLER
kaka zake na dada zake wote walikufa wangali wachanga akiwa na umri wa miaka sita
familia yake ilihamia Passau huko ujerumani na baadaye tena 1894 ikahamia leonding
hata hivyo mwaka 1895 Alois alistaafu kazi yake huko Hafeld ambako akawa mkulima
na mfugaji wa nyuki. Shughuli za kilimo na ufugaji zilifeli vibaya sana na familia ya
hitler ililazimika kuhamia Lambach, Hitler alianza kujifunza kuimba nyimbo za dini
kanisani na alidhamiria kuwa muhubiri, mwaka 1898 familia yake ilihamia makazi ya
kudumu LEONDING,
NYUMBA ALIYOISHI ADOLFU HITLER AKIWA HUKO LEONDING
Mnamo mwaka 1900 mdogo wake Hitler Edmund alikufa kwa ugonjwa
wa SURUA kifo ambacho kilimuathiri sana jambo lililopelekea Hitler kubadilika kitabia kwa
sehemu kubwa akawa mbishi, mtundu na akadiliki kupigana na baba yake na walimu wake
tofauti na awali ambapo alikuwa ni mtoto mtiifu na mwelewa, baba yake alipata mafanikio
makubwa katika shughuli za usimamizi wa mila na desturi[chifu] jambo amabalo alitaka
mwanaye Adolf Hitler afuate nyayo zake jambo ambalo lilipingwa vikali na mwanae ambaye
alitaka apelekwe kwenye shule ya sanaa hii ilipelekea kutokea tofauti kubwa kati yao. Mwaka
1900 Alois Hitler alimpelekea mwanae katika shule ya secondari iliyojulikana kwa jina la
REALSCHULE ambapo hitler alikubali kwa shingo upande na akafeli vibaya sana ktk mitihani
yake hii alifanya makusudi kwa kujua kuwa baba yake akiona maendeleo yake mabovu
shuleni angebadili uamuzi wake na kumpeleka mwanae katika shule ambayo ni ndoto yake[sanaa]
na hivyo kushindwa kuendelea na masomo
kama vijana wengi wa kijerumani, Hitler alianza kushika asili na desturi za kijerumani
ambazo kwa kipindi hicho ilikuwa ni ya kibaguzi, Hitler na marafiki zake walianza kutumia salamu
ya kijerumani[HEIL] na kuimba nyimbo za kijerumani badala ya zile za AUSTRALIA, Baada ya
kifo cha baba yake kilichotokea 3,january/1903 maendeleo ya kitaaluma kwa Hitler yaliendelea
kuzorota kwa kasi na baadaye mama yake alimuondoa kwenye shule hiyo
Kutoka mwaka 1905 Hitler aliishi na mama yake yakiwa maisha mapya baada ya baba yake
kufariki, mwanzo alifanya kazi ndogondogo na baadaye akawa anafanya kazi za upakaji rangi ikiwa
ni pamoja na kuchora, kuuza rangi za maji nk.
MOJA YA MAJENGO YALIYOPAKWA RANGI ZA MAJI NA ADOLF HITLER ENZI ZA UHAI WAKE
alidhamiria kuendeleza kipaji chake cha sanaa kwa
kuomba kujiunga na chuo cha VIENNA,S ACADEMY OF FINE ART lakini alikataliwa kwa mara ya
kwanza 1907 na baadaye akakataliwa tena 1908, kiongozi wa chuo alitoa maoni kuwa Hitler alikuwa
na uwezo mkubwa katika uchoraji lakini hakuwa na sifa za kitaaluma yenye ushahidi kwakuwa
hakuwa na cheti cha kuhitimu elimu ya secondari. Mnamo 21/12/1907 mama yake Clara Hitler
akiwa na umri wa miaka 47 alifariki kwa ugonjwa wa kansa ya titi, kifo cha mama yake kilisababisha
mfumo wa maisha yake kuyumba na kulazimika kupoteza lengo la kusoma kichwani mwake na
akaanza maisha mapya kwa kutafuta kazi za vibarua kwa ajili ya kujikimu, maisha hayo yalifanya
kuwa mtoto wa mitaani asiye na pa kukaa. Kwa muda ambao Hitler alikuwepo VIENNA kulikuwa
na chuki za kidini pamoja na ubaguzi wa rangi, hofu ya kuchukuliwa kama mkimbizi kutoka mashariki
ilitwala na kuenea kwa kasi. Hitler alipendelea kusoma magazeti ya DEUSCHES VOLKBLATT
ambayo yalivumisha chuki kwa wakristo ambapo hitler alikuwa ni mmoja wao
Mei,1913 Hitler alikabidhiwa shamba lake ambalo lilikuwa ni urithi wa marehemu baba yake
na alihamia MUNICH kukwepa kujiunga na jeshi la Australia hii ni kwasababu jeshi hilo lilikuwa
na mchanganyiko wa jamii tofautitofauti jambo ambalo hakulipenda Hitler.
Katika VITA YA KWANZA YA DUNIA, Hitler alikuwa akiishi MUNICH na alijitolea kulisaidia jeshi
la BAVARIA akiwa kama ni mwananchi wa Australia na aliwekwa kwenye kikundi cha RESERVE INFANTRY
REGIMENT namba 16 combania namba 1
HITLER NA RAFIKI ZAKE WA KIKOSI CHA RESERVE INFANTRY REGIMENT
na alikuwa kama mpeleka taarifa kikosi cha magharibi
ya mbele Ufaransa na Ubelgiji na muda wote alikuwa nyuma ya mstari wa kikosi kilichokuwa mbele
ya mapigano vikosi alivyotumikia wakati huo ni kikosi cha YPRES, SOMME, ARRAS na PSSCHENDAELE
na alijeruhiwa bega la kulia alipokuwa SOMME. Alifanya kazi kwa juhudi kubwa na baadaye akatunukiwa nishani
ya msalaba wa chuma na akapanda cheo kuwa PRIVATE, mwaka 1918 Kwa amri ya Lieutenant
Hugo Gutmann, Hitler alitunukiwa nishani ya chuma daraja la kwanza na kupandishwa cheo kuwa COPLO.
KUINGIA SIASA
Baada ya vita alikosa kazi lakini aligundua kipawa chake cha kuhutubia watu, akajiunga na siasa
na kuingia katika chama kidogo cha Nazi alikopanda ngazi haraka.
KADI YA HITLER YA CHAMA CHA DAP
JARIBIO LA MAPINDUZI
Hitler alivutwa sana na mfano wa Benito Mussolini kiongozi wa kifashisti wa Italia
aliyefaulu mwaka 1922 kupindua serikali ya Italia kwa maandamano makubwa ya
wafuasi wake kuelekea Roma Mwaka 1923 Hitler alijaribu kumwiga Mussolini kwa kupindua
serikali ya Bavaria - kama utangulizi wa kupindua serikali ya kitaifa
huko Berlin - lakini alikamatwa na kuhukumiwa kwa uasi huo kifungo cha miaka
mitano, ingawa alitumikia miezi tisa tu. Chama chake kilipigwa marufuku.
BENITO MUSSOLIN WAKIWA NA ADOLF HITLER KWENYE MKUTANO WA HADHARA
Hitler akiwa kijana aliwahi kusoma vitabu vya Mwingereza Chamberlain aliyedai kwamba
kuna aina mbalimbali za watu wenye tabia na thamani tofauti sana.
Akiwa gerezani aliandika kitabu kilichoitwa "Mein Kampf("Mapambano Yangu")
alikojaribu kueleza imani na siasa zake. Humo alieleza pia chuki dhidi ya Wayahudi
na itikadi yake ya ubaguzi wa kimbari. Katika itikadi hiyo mbari ya juu ni watu
wa Ulaya ya Kaskazini aliowaita "Waaria na wale ambao ni
duni zaidi ni watu weusi. Vikundi vingine vimo katikati. Lakini watu
wabaya kabisa katika itikadi hiyo ni Wayahudi ambao ni wajanja wakuu
upande mmoja, lakini hawana uwezo wa kuunda kitu kwa upande mwingine.
Hivyo wanajaribu kwa ujanja wao kutawala dunia kwa kuiba fikra na mafanikio ya Waaria.
Kujenga chama
Baada ya kutoka gerezani alirudia siasa. Alijitahidi kushika utawala wa chama cha
NSDAP akakubaliwa kuwa kiongozi mkuu. Ndani ya chama alianzisha vikosi viwili
vilivyovaa sare vikifanya mazoezi kama wanamgambo na kuwa tayari kupigana na
maadui wa kisiasa wakati wa maandamano.
Kikundi cha SA ("Sturmabteilung" - "Kikosi cha kushambulia") kilikuwa na watu wengi
sana kikavuta hasa wanaume wasio na kazi waliovaa sare ya kahawia Kikosi cha pili
kilikuwa na watu wachache kikaitwa "SS " ("Schutzstaffel" - "Kikosi cha ulinzi") waliovaa sare nyeusi.
Chama chake hakikufaulu hadi 1929 , wakati uchumi wa dunia pamoja na wa Ujerumani
ulipoporomoka vibaya katika mdodoro mkuu Mamilioni waliachishwa kazi na kuona
njaa . Katika hali hiyo watu walianza kupigia kura vyama vyenye itikadi kali.
Katika uchaguzi wa mwaka 1930 kura za NSDAP ziliongezeka
kutoka 2.6% hadi 18.3%. Serikali za Ujerumani zilikuwa za vyama vingi na
dhaifu. Mwaka 1932 chama cha NSDAP kilipata 33% za kura na kuwa
chama chenye kura nyingi zaidi nchini na chama kikubwa katika bunge
. Katika hali hiyo viongozi wa Dola la Ujerumani waliamua kumwingiza
Hitler katika serikali mwaka 1933.
Chansela na kiongozi wa Ujerumani
Tarehe 30 Januari Hitler akawa Chansela wa Ujerumani. Mara moja alichukua nafasi
kuwakandamiza wapinzani wake na baada ya mwaka mmoja hata wale waliomwingiza
madarakani. Baada ya mwaka mmoja utawala wake ulisimama imara kabisa ilhali
wapinzani wengi walikamatwa na kupelekwa katika makambi ya KZ
Hitler alifuata siasa ya kujenga uchumi na kurudisha watu kazini
akibahatika kwamba uchumi wa dunia ukapaa tena.
ADOLF HITLER MUDA MFUPI BAADA YA KUAPISHWA KAMA KANSELA WA UJERUMANI
Hitler alifuta mapatano yote ya Ujerumani yaliyoweka mipaka kwa ukubwa
wa jeshi lake kuwa watu 100,000 tu akajenga jeshi kubwa zaidi, akaanzisha utawala
wa kidikteta wa "Dola la Tatu akipiga marufuku vyama vya upinzani
. Alitesa wapinzani wote na watu wa mbari alizochukia, hasa Wayahudi
Siasa dhidi ya Wayahudi
Chuki dhidi yaWajerumani waliokuwa Wayahudi aliionyesha kwa sheria mbalimbali
zilizokuwa kali zaidi na zaidi. Idadi ya Wayahudi katika Ujerumani ilikuwa ndogo,
takriban nusu milioni kati ya wakazi milion62. Kila Mjerumani akitaka kuajiriwa na
serikali au kupata nafasi ya masomo alitakiwa kuorodhesha wazazi na mababu hadi
kizazi cha pili. Kwanjia hiyo Hitler alipanga Wajerumani wote katika vikundi vya "Waaria
(ambao hawana Wayahudi katika familia), "Wayahudi" (watu wenye asili ya Kiyahudi, hata
kama wameshakuwa Wakristo tangu vizazi kadhaa au hawakufuata dini "Wayahudi nusu"
kama mzazimmoja alikuwa Myahudi, "Wayahudi robo" kama mmoja kati ya mababu na
mabibi wanne alikuwa Myahudi. Wayahudi na Wayahudi nusu walifukuzwakatika ajira ya
serikali na walikataliwa kufanya kazi mbalimbali.
MAITI ZA WAYAHUDI WALIOUAWA KWA AMRI YA ADOLF HITLER
AMRI YA KUWACHOMA MOTO WAYAHUDI ILIYOSAINIWA NA ADOLF HITLER SEPT 1 1939
Sheria kuhusu "Aibu wa mbari" ilikataza ndoa kati ya "Waaria" na "Wayahudi"; "Wayahudi"
waliondolewa uraia kamili. Tokeo moja la siasa hiyo lilikuwa kuondoka kwa Wayahudi wengi kidogo
katika Ujerumani; baada ya mashambulizi makali na mauaji mwaka 1938
mwelekeo huo uliongezeka. Hasa wanasayansi na wasanii wengi
walihamia nchi huru.
Siasa yake katika mwaka 1939 ilisababisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia
Hitler alifuata mwanzoni siasa ya kukusanya Wajerumani wote wa Ulaya
katika Dola la Ujerumani. Mwaka 1938 alifaulu kuteka Austria na
maeneo ya Wajerumani katika Ucheki bila upingamizi wa
kimataifa.
Lakini aliposhambulia Poland tarehe 1 Septemba tendo hili lilikuwa mwanzo wa Vita
Kuu ya Pili ya Dunia kwa sababu Uingereza walisimama imara kwa mikataba ya kusaidiana na Poland.
Wakati wa vita Hitler alichukua mwenyewe uongozi mkuu wa jeshi. Mwanzoni
alifaulu hata dhidi ya ushauri ya majenerali wake, hasa wakati wa vita
dhidi ya Poland na Ufaransa. Lakini maazimio yake ya 1941 ya kushambulia
Urusi na kutangaza hali ya vita dhidi ya Marekani
yalikuwa mwanzo wa mwisho wake. Nguvu ya kiuchumi wa
Ujerumani haikutosha kushindana na dunia yote.
Wakati wa vita aliamuru uuaji wa Wayahudi wote wa Ulaya na inakadiriwa
alifaulu kuwaua takriban milioni sita (2/3 ya Wayahudi wote wa Ulaya)
pamoja na watu vya mbari mbalimbali kama Wasinti
(kati ya 200,000 na 1,500,000).
Hasa alipoona ya kwamba vita dhidi ya Urusi haikufaulu haraka jinsi
alivyotegemea aliamua kumaliza jambo lililosababisha chuki yake hasa.
Azimio la "usuluhisho wa mwisho wa suala la Kiyahudi" lilichukuliwa
mwisho wa mwaka 1941 na kutangazwa mbele ya viongozi
wachache mnamo Januari 1942 katika Mkutano wa Wannsee
Baadaye siasa ya kuwatenda Wayahudi vibaya na kuwaua katika maeneo
fulani ilibadilishwa kulenga Wayahudi wote katika nchi zote zilizokuwa
chini ya athira ya Ujerumani au kutekwa na jeshi lake. Hadi mwisho wa
vita Wayahudi walikusanywa kutoka kote Ulaya na kupelekwa kwa reli
hadi makambi ya mauti
Mwisho wa vita na kifo
Maafisa wa jeshi ya Ujerumani walipanga mara kadhaa kumwua Hitler lakini hawakufanikiwa.Tarehe
20 Julai alijeruhiwa na bomu ya Stauffenberglakini hakuuawa.
Mwishoni mwa vita Hitler alikaa Berlin hadi jeshi la Kirusi lilipokuwa limeshaingia mjini.
Tarehe 30 Aprili alijiua kwa sumu pamoja na mpenzi wake Eva
(alimwoa masaa tu kabla ya kujiua) na mbwa wake mpendwa "Blondi
Maiti zilichomwa kwa petroli lakini zilitambuliwa na Warusi
kutokana na meno yake.
ADOLF HITLER AKIWA NA MKEWE PAMOJA NA MBWA WAKE ALIYEMPENDA SANA NA AMBAYE WALIKUFA PAMOJA.

Subscribe to:
Comments (Atom)